Genesis 31:44-49

44Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.”

45Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. 46Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. 47Labani akaliita Yegar-Sahadutha
Yegar-Sahadutha maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiaramu.
na Yakobo akaliita Galeedi.
Galeedi maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiebrania.

48Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. 49Pia liliitwa Mispa,
Mispa maana yake Mnara wa ulinzi.
kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.
Copyright information for SwhKC